Alhamisi ya July 13, 2017 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam iliandikwa historia mpya baada ya Klabu ya Everton inayocheza Ligi Kuu ya England EPL kucheza kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania wakicheza dhidi ya Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya.
Katika mchezo huo Everton walishinda kwa mabao 2-1 yaliyofungwa na Wayne Rooney na Kieran Dowell huku bao la Gor Mahia likifungwa na Jacquies Tuyisenge.