Michezo

Timu zenye thamani kubwa zaidi duniani zimetajwa na FORBES

By

on

Jarida maarufu la Forbes limetoa list nyingine timu za michezo mbalimbali zenye thamani kubwa zaidi duniani ambapo club ya Dallas Cowboys imetajwa kuongoza ikifatiwa na timu ya Basketball ya New York Yankees na nafasi ya tatu imeshikwa na club ya soka ya Manchester United.

Kwa tafsiri hiyo ni kwamba Manchester United ndiyo club ya soka yenye  thamani kubwa zaidi duniani ambapo iliongoza pia mwaka 2011 na 2012 ikitajwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.69 ikifatiwa na Barcelona yenye thamani ya dola bilioni 3.64 na Real Madrid ikiwa na thamani ya dola bilioni 3.58.

Kiujumla ni kwamba, ndani ya list ya timu 50 zenye thamani zaidi duniani, kuna timu 7 za soka zikiwemo Bayern Munich inayoshika nafasi ya 15 ikwia na thamani ya dola bilioni 2.71, Manchester City wako nafasi ya 35 wakiwa na thamani ya dola bilioni 2.083; Arsenal wako nafsi ya 43 wana thamani ya dola bilioni 1.93 na Chelsea wako nafasi ya 46 wakiwa na thamani ya dola bilioni 1.845.

Nimekuwekea hapa chini list ya timu 10 zenye thamani zaidi duniani.

  1. Dallas Cowboys – ($4.2bn).
  2. New York Yankees – ($3.7bn).
  3. Manchester United – ($3.69bn).
  4. Barcelona – ($3.64bn).
  5. Real Madrid – ($3.58bn).
  6. New England Patriots – ($3.4bn).
  7. New York Knicks – ($3.3bn).
  8. New York Giants – ($3.1bn).
  9. San Francisco 49ers – ($3bn).
  10. Los Angeles Lakers – ($3bn).

VIDEO: Gor Mahia VS Everton, Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017), Bonyeza play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments