July 16, 2017 millardayo.com imekukusanyia uchambuzi wa magazeti kutoka twitter @millardayo ikiwa ni uchambuzi wa Habari zote kubwa kupitia magazeti yaliyoandikwa leo Tanzania na hizi ni baadhi ya Habari kubwa zilizoandikwa leo.
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya Kidato cha Sita ambapo zipo shule 10 zilizofanya vizruri na zilizofanya vibaya pia hazijakosekana huku matokeo jumla yakipanda kwa 0.59% na wasichana wakionesha kufanya vizuri zaidi ya wavulana.
2/2 Shule 10 za mwisho
6 Meta – Mbeya
7 Mlima Mbeya – Mbeya
8 Mbeya Sec – Mbeya
9 Al-Ihsani Girls – Unguja
10 St Vincent – Tabora#HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
1/2 Shule 10 za mwisho
1 Kiembesamaki – Unguja
2. Hagafilo – Njombe
3. Chasani – Pemba
4. Mwenyeheri – DSM
5. Ben Bella – Unguja#HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
2/2 Shule 10 bora:
6. Mzumbe – Moro
7. St Mary's – Mazinde juu Tanga
8. Tabora Boys – Tabora
9. Feza Boys – DSM
10 Kibaha – Pwani#HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
1/2 Shule 10 bora:
1. Feza Girls – DSM
2. Marian Boys – Pwani
3. Kisimiri – Arusha
4. Ahmes – Pwani
5.Marian Girls – Pwani#HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
TBS imetangaza kiwango cha ubora kinachopaswa kutumiwa kwa sare za Shule au Taasisi ili kudhibiti kasoro zinazolalamikiwa. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Waziri wa Sheria Prof. Kabudi amewataka viongozi kushughulikia suala la rushwa ndani ya Mahakama bila woga wala upendeleo. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Mahujaji zaidi ya 2,500 wa Tanzania wanatarajiwa kwenda Makka, Saudi Arabia kushiriki Ibada ya Hijja mwaka huu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk. Hassan Abbas ameteuliwa kuongoza Kamati ya kuchunguza ubia kati ya TBC na StarTimes. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Wazazi, walezi wa watoto walemavu wameonywa kuacha kuwatumia kuomba mitaani badala ya kuwasomesha ili waondokane na umasikini #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
RC Njombe amebatilisha agizo la Halmashauri ya Wilaya Makete kuwataka wafanyabiashara kufunga maduka na kuhamia ofisi za Kata #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imetakiwa kuhakikisha viwanja vilivyoboreshwa vinajisimamia na kujiendesha vyenyewe. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Wanafunzi 47 wa Shule za Msingi na Sekondari wilayani Serengeti, Mara wamekatisha masomo kwa ujauzito Jan 2016 hadi Jun, 2017. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
TRA imeongeza muda wa kupokea kodi za majengo za mwaka 2016/17 hadi July 31, 2017 na itatoa adhabu kwa atakayekaidi agizo hilo. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
TRA imewataka wamiliki wa vituo vya mafuta waache visingizio na watekeleza agizo la kununua na kufunga mashine za risiti za EFPP. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Mkazi wa Tambukareli Shinyanga mjini, Sarah Bundala (55) amejinyonga kwa kinachodaiwa kukimbiwa na rafiki aliyemdhamini mkopo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Wananchi 251 wa mitaa 3 ya Bwiru ya Elimu, Ziwani, Prace wametishia kuishtaki Halmashauri ya Ilemela kwa madai ya kuwapora maeneo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
RC Makalla amewaonya Maofisa Mifugo Wilaya za Chunya na Mbarali, Mbeya kuepuka na vitendo vya rushwa wakati wa kupiga chapa mifugo. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Naibu Spika Dk Tulia, Mbunge wa Viti Maalum Dodoma, Mariam Mzuzuri wamewapa mbinu wanafunzi wa kike za namna ya kukwepa vishawishi. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), limetangaza matokeo ya Kidato cha Sita huku ufaulu ukishuka ukilinganisha na mwaka uliopipa. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Viongozi 6 wa CHADEMA akiwemo Katibu Mkuu na wabunge wawili wanashikiliwa na Polisi Ruvuma wakidaiwa kufanya mkutano bila kibali. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
Katibu Mkuu wa CHADEMA kawekwa ndani saa 48!!!