Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu alisema amepata taarifa kwamba unafanyika utaratibu wa kumpeleka Mahakamani Edward Lowassa, sasa kisheria Waziri mkuu huyo mstaafu anayo kinga?
Tundu Lissu amesema “Nimeambiwa jiandaeni, Mh. Lowassa atapelekwa Mahakamani kushtakiwa kwa uchochezi kwa kuzungumzia maswala ya uonevu wanaofanyiwa Mashehe wa uamsho, swali ni je… kinga ya viongozi ikoje?”
“Mtu pekee kwa mujibu wa sheria za Tanzania ambae ana kinga dhidi ya mashtaka ya jinai ni JPM peke yake, katiba yetu inasema Rais ndio mwenye kinga dhidi ya mashtaka ya jinai lakini wengine wote kuanzia Makamu wa Rais mpaka Karani wa Mahakama ya Mwanzo Ikungi kwetu hawana kinga ya kushtakiwa”
“Endapo Mh. Lowassa atapelekwa Mahakamani, hatoweza kusema nina kinga niliwahi kuwa Waziri Mkuu” – Tundu Lissu
Mtazame zaidi hapa chini kwa kuplay hii video
VIDEO: “Utaratibu unafanywa wa kumpeleka Mahakamani Edward Lowassa” – Tundu Lissu, mtazame mwanzo mwisho hapa chini