Habari za Mastaa

Uliamini Flora ndio kasema Mwanaume aseridhisha aachwe? ‘sitakaa kimya tena’

on

Siku kadhaa zilizopita kulikuwa na taarifa ambazo zilikua na kichwa cha habari mitandaoni zikimnukuu mwimbaji wa Injili Tanzania ambaye aliwahi pia kuwa mke wa Emmanuel Mbasha, Madam Flora akisema “Hakuna haja ya kuwa na Mwanaume asiyekuridhirisha kinyumba.”

Sasa leo July 19, 2017 Ayo TV na millardayo.com zimempata mwimbaji huyo ambaye ameikataa kauli hiyo na kusema hajasema kitu cha namna hiyo >>>”Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na radio yoyote na kuzungumza maneno hayo, naomba mzipuuze maana ni mpuuzi mmoja tu ameamua kuonyesha upuuzi wake na kutafuta followers kwenye page yake”

“Na niseme tu kwamba hivi sasa sitakaa kimya tena, huyo aliyezoea kunizushia story za uongo akifikiri siijui sheria ajipange vizuri maana Mahakama ipo na sheria ipo” – Madam Flora.

Flora Mbasha kaolewa tena… Tazama ndoa ilivyofungwa!!!

Soma na hizi

Tupia Comments