Leo ni July 19, 2017 ambapo millardayo.com imekukusanyia na kukusogezea story zote kubwa kwenye magazeti ya Tanzania asubuhi ya leo ambapo kuna stori kadhaa kubwa zilizopewa uzito wa hali ya juu.
Miongoni mwa story kuwa leo ni pamoja na Serikali kumtaka Mwanasheria wa CHADEMA na Wakili wa Mahakama Kuu Tundu Lissu kutumia weledi na kuacha kupiga propaganda. Mmiliki wa IPTL kuendelea kulipwa Tsh. 5.9 bilioni licha ya mitambo yake ya kufua umeme kuzimwa.
Serikali imewaonya Watumishi wa Umma wanaotoa siri za Serikali na kuzisambaza mitandaoni kuwa watachukuliwa hatua za kisheria. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Polisi Morogoro inawashikilia watu 9 kwa tuhuma tofauti akiwemo mmoja anayetuhumiwa kumuua mkewe kwa kitu chenye ncha kali. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema ushindi wa Rais Magufuli katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 ni wa uhakika 100%. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua ripoti ya kwanza ya Utawala Bora iliyoandaliwa chini ya mpango wa APRM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Polisi Temeke limefanikiwa kuwakamata watu 11 wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi wa mali zinazosafirishwa ndani na nje ya nchi. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Ofisa wa Polisi Koplo Brayson amedai Salum Njwete 'Scorpion' alitumia vidole kumtoboa macho Said Mrisho na kumjeruhi kwa kisu. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Mfanyabiashara Harbinder Sethi ataendelea kulipwa Tsh. 5.9bilioni mwezi huu licha ya kuwekwa rumande na mitambo yake kuzimwa. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili Prof. Lipumba ameomba ulinzi baada ya kuzinduliwa operesheni maalum kumuondoa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Serikali imemshauri Tundu Lissu kutekeleza wajibu kusimamia weledi akiwa Wakili wa Mahakama Mkuu badala ya kufanya propaganda #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Polisi wilayani Nyasa, Ruvuma limeongeza tuhuma kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji akidaiwa kutoa lugha ya kuudhi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Viongozi wa kisiasa, Serikali na kidini walijitokeza ktk ibada ya kuuaga mwili wa mke wa Waziri Mwakyembe iliyofayika KKKT. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Watanzania wameshauriwa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuhakikisha wanasaidia makundi yasiyojiweza. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Serikali imesema imejipanga kutatua vikwazo vilivyopo katika soko la Afrika Mashariki na kuhakikisha vijana wanaingiza bidhaa zao. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
BAKWATA limevitaka vyombo vya dola kumchukulia hatua kisheria Hamis Issa ambaye anajiita Mtume wakati akijua ni upotoshaji. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Polisi Z'bar imeagizwa kuwasaka na kuwakamata watu waliohusika kumshambulia kwa mapanga utingo wa daladala Khamis Mgaya Juma. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Jeshi la Polisi Z'bar limesema litamfikisha Mahakamani dereva wa gari walimofia watoto wanne baada ya kukamilisha upelelezi. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Familia 18 hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba waliyokuwa wamepangisha kuteketea kwa moto katika kijiji cha Ngarenairobi, Siha. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Licha ya kuwa na 80% ya nguvukazi kwenye kilimo, Afrika inakadiriwa kutumia Tsh. 248.6trilioni ifikapo 2025 kuagiza chakula nje. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Wakazi wawili wa Kilewani, Kasanga wilayani Kalabo, Rukwa wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye Ziwa Tanganyika wakivua samaki. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Mayala John (47), mkazi wa Uvinza, Kigoma amefikishwa Mahakamani kwa kumbaka mtoto wa kufikia mwenye miaka 13 na kumpa ujauzito. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Serikali imesema itawalipa fidia kwa mujibu wa sheria wananchi wote waliopisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Upungufu wa wataalamu wa magonjwa ya moyo ktk Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ni kikwazo cha kupanua mtandao wa huduma. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
IGP Sirro ameendelea kufanya mabadiliko ktk Jeshi hilo akimuhamisha Kamanda wa Polisi Kinondoni SACP S. Kaganda kwenda Makao Makuu. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Serikali imezikataa zaidi ya Tsh 40m zilizowekwa ktk akaunti ya TRA July 10, 2017 na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Ngeleja #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
Ayo TV MAGAZETI: Uchambuzi wa Magazeti ya Tanzania leo July 19, 2017…bonyeza PLAY kutazama kwenye VIDEO hii!!!
Uwaziri Mkuu utazuia Lowassa asipelekwe Mahakamani? Lissu afunguka…tazama kwenye VIDEO hii!!!