Mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye anakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi leo July 19, 2017 ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na hali yake ya afya kutokuwa nzuri.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Wakili mwandamizi wa serikali Nassoro Katuga àlidai amepata taarifa kutoka kwa Daktari wa Magereza kuwa Manji ni mgonjwa hivyo amepelekwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ‘JKCI’ iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha, alidai Mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika lakini upo katika hatua ya mwisho hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi siku nyingine ambapo Hakimu Shaidi alikubali kuiahirisha kesi hadi August 4, 2017.
Hata hivyo Washtakiwa wenzake Ofisa Rasilimali watu, Deogratias Kisinda, msimamizi wa Stoo Abdallah Sangey na Msaidizi Mkuu wa Stoo Thobias Fwele wamefika Mahakamani.
Yusuf Manji anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ameshindwa kufika Mahakamani kutokana na kupelekwa JKCI Hsptl wenzie wamefikishwa Kisutu pic.twitter.com/8atFwt9fku
— millardayo (@millardayo) July 19, 2017
ULIPITWA? Mashtaka 7 aliyosomewa Yusuf Manji akiwa Hospitali…hii VIDEO ina kila kitu PLAY kutazama!!!
VIDEO: Yusuph Manji baada ya kutajwa na RC Makonda kwenye sakata la dawa za kulevya, tazama hapa chini kwenye hii video
VIDEO: Yusuph Manji alivyotolewa Hospitali na kupelekwa Mahakamani Feb 2017, bonyeza play hapa chini kujionea