Kesi kadhaa za uhujumu uchumi zimeendelea kutikisa ambapo leo July 19,2017 watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi wa zaidi ya Tsh. Bilioni 24.
Wakisomewa makosa yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mwambapa, Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga alisema Safina Rupia na David Chamwino wanakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi kwa zaidi ya Tsh. Bilioni 24.
Wakili Katuga alidai kati ya July 11, 2015 na October 28, 2015 katika Bandari kavu ya Azam, Sokota Temeke DSM, waliisababishia TRA hasara ya Tsh. Bilioni 12.6 kwa kuondoa Makontena 329 bila kulipiwa kodi katika Bandari hiyo.
Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi July 27, 2017 huku Washtakiwa wakikosa dhamana kutokana na Mahakama kutokuwa na mamlaka.
Ukisikia kutakatisha Fedha na kuhujumu Uchumi, hii ndio maana yake…tazama kwa kuplay VIDEO hii!!!
William Ngeleja kurudisha fedha za ESCROW, Sheria ya TZ inasemaje? play hapa chini kuelezewa zaidi