Teknolojia inazidi kukua ambapo sasa hivi kwenye maonyesho ya CES (Consumer Electronic Show) huko Las Vegas Marekani kumeonyeshwa printer mpya yenye uwezo wa ku-print vitu vinavyoweza kuliwa na binadamu.
Mfano mzuri wa kitu kilichokuwa printed ni chocolate yenye umbo ambalo ingekuwa ni kazi kubwa kutengenezwa kwenye hali ya kawaida ambapo watengenezaji wake wanasema printer hii inaweza kutumika kwenye Restaurant na kwengine.
Version yake ya kwanza inaweza kuwa na gharama ya dola 5000 na advanced one inaweza kuwa na bei yake mara mbili na watengenezaji wanakwambia wana printer ambazo zinaweza ku-print vitu vya plastic kwenye 3D ambazo zinaweza kuwa na gharama ya dola 5,000.
Printer ya kawaida inawekwa karatasi lakini printer hii inawekwa material ya kitu unachotaka kutengeza, yani kama unataka kutengeneza chocolate unaweka material ya kutengenezea chocolate.
Tazama hapa chini ni video ya ripoti ya BBC na uone jinsi chocolate inavyotengezwa kwenye printer.