July 27, 2017 moja ya stori iliyoandikwa kwenye Magazeti ya leo ni pamoja na Mkazi wa Ilemela, Mwanza, Makusudi Rashidi mwenye umri wa miaka 39, kushikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi ambaye ni mdogo wake mwenye umri wa miaka 11.
millardayo.com tayari imekukusanyia na kukusogezea uchambuzi wote wa Magazeti ya leo July 27, 2017 kutoka kwenye twitter yangu @millardayo.
Mkazi wa Ilemela, Mwanza, Makusudi Rashidi (39), anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumbaka mwanafunzi (11) ambaye ni mdogo wake. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Wabunge 8 waliovuliwa uanachama na Chama cha Wananchi, CUF wamepiga hatua hiyo na kutishia kwenda Mahakamani kutafuta haki yao. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mfanyabiashara mwanamke Mariam Omary (31), mkazi wa Muharakani, Kibaha, Pwani ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inachunguza makontena 10 yaliyokamatwa bandarini na kemikali bashirifu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema hatoshiriki siasa za vurugu kupinga mipango ya Serikali ya Rais JPM kuleta maendeleo. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Watanzania wametakiwa kutumia kikoa cha rajisi ya dot tz ya mtandao wa internet kinachomilikiwa na Tanzania badala ya nchini nyingine #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Wazalishaji wa nguzo za umeme wameiomba TANESCO kuachana na mpango wa kuhamia katika matumizi ya nguzo za zege. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mkazi wa Kwimba, Mwanza Limi Bunzama amefariki dunia baada ya kutafunwa na fisi alipokuwa anacheza karibu na mama yake. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Edward Lowassa leo ametimiza miaka miwili tangu kuweka historia ya kuwa kiongozi wa kwanza ngazi ya juu serikalini kuhama CCM. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Wakazi kijijini Undomo, Nzega wameyakimbia makazi yao baada ya wanawake watano kuuawa kwa kuchomwa moto kwa imani za kishirikina. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Baada ya Mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba kuwavua uanachama Wabunge 8, Spika Ndugai amesema hawana sifa kuendelea kuwa Wabunge. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Chuo cha Kimataifa cha Kampala, Kiu-DCC kimepandishwa hadhi, kitaitwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KiuT) #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Jeshi la Polisi Tanga likishirikiana na TRA wamekamata shehena ya bidhaa za magendo sukari na mafuta ya kupikia zikitokea Pemba. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amewaonya walimu wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi, akiwataka kuacha haraka. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Imeelezwa kitendo cha baadhi ya wanawake kuwanyanyasa waume zao kwenye ndoa ikiwemo kuwapiga ni moja ya sababu ya kutelekezwa. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Hatima ya Mbunge Tundu Lissu ya ama kutoka au kubaki mahabusu inatarajia kujulikana leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
"Mtu yeyote anaweza kuondoka, lakini CHADEMA kama Taasisi itabaki imara." – Freeman Mbowe. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
"Si sahihi Polisi kuwazuia waandishi wanapotimiza majukumu yao." – IGP Simon Sirro. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA), imekata maji ktk Chuo cha Mafunzo ya Polisi (CCP), wakidai Tsh. 523 milion. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mahakama Kuu DSM inatarajia kusikiliza maombi ya dhamana dhidi ya Yusuf Manji anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi August 4. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Wakati madiwani Arusha wakihama CHADEMA, Mwenyekiti wake Mbowe amesema mtu anaweza kuhama ila chama kama Taasisi kitabaki imara. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Madalali 4 wa madini wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwaumiza macho kwa kemikali baada ya kutofautiana na madalali wenzao. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Chato, Geita, imeamuru viongozi 51 wa CHADEMA kuachwa kwa dhamana baada ya kukaa mahabusu tangu July 7. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017
Mganga wa jadi Levocatus Kanjalanga (65) ameuawa kwa kuchomwa mkuki mgongoni na mtu anayedaiwa ni mteja wake wa muda mrefu. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 27, 2017