Ni kweli kwa kipindi kirefu kwenye ardhi ya Tanzania tumezoea kwenda kwenye sehemu zilezile za starehe kama vile beach na bar lakini ni furaha yangu kwa sasa kuona vijana wa Kitanzania walioamua kutumia ubunifu wao kuleta kitu tofauti wanafanikiwa kwenye hii ya BBALL Kitaa.
Mkusanyiko hutokea mara kwa mara popote penye uwanja wa basketball, mechi inachezwa, msosi na vinywaji vinapatikana, marafiki mnakutana na wakati wote huu muziki unasindikiza, kingine kilichonivutia ni kwamba sasa hivi inakua kama ‘outing’ flani hivi yani uwanja upo ufukweni, ulinzi na usalama vinazingatiwa.
Sasa basi, zifuatazo ni picha za BBALL Kitaa chini ya mataa iliyofanyika kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2014 Januari 10 kwenye viwanja vya Gymkhana ambapo CBE na UDSM walikua wanakipiga.
CBE ndio wameshinda
Hizi ni baadhi ya picha zikionyesha jinsi Bball kitaa ilivyokua.
Reuben Ndege, namfahamu kama mwanzilishi wa hii event ambayo siku hadi siku inazidi kuchukua zake headlines.