Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameporomoka kwenye nafasi za watu tajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51. Kwa mujibu wa Jarida la Forbes limeripoti kwamba utajiri wa Dangote umepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushuka thamani kwa pesa ya Nigeria.
Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa Cement, Sukari, na Unga wa Ngano, alikua kwenye headlines zaidi mwaka 2016 baada ya kutangaza kuinunua club ya Arsenal miaka minne ijayo. Jana Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpita Bill Gates kwa masaa manne kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya tatu.
Nimekuwekea hapa top 10 ya matajiri wa dunia kwasasa.
Namba zinabadilika tena, Forbes wameitaja list mpya ya matajiri wa dunia, Bill Gates ametetea nafasi yake, Buffet amerudi No. 2, Jeff No. 3. pic.twitter.com/hTZLgGMPmJ
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
VIDEO: Kama ulizoea kununua chakula kwa 5000, sasa utanunua kwa 3500. Bonyeza play kutazama