Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza mipango ya Serikali katika kukabiliana na homa ya Ini akisema chanjo ya homa hiyo itapatikana kwa wananchi wote waliokuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo au walioupata ugonjwa huo bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha hadi kufikia 2020 kutoka mwaka wa fedha 2018/2019.
Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa hakuna mlipuko wa ugonjwa huo lakini ametoa angalizo kuwa Wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki wapo katika hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo.
>>>”Sasa hivi hakuna ushahidi wa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Ini, hata hivyo Wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu.” – Waziri Ummy.
EXCLUSIVE: David Kafulila aitwa Marekani…tazama kila kwenye hii video kwa kubonyeza play.