Baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ‘TCU’ kutangaza mabadiliko na kuurejesha Udahili wa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwenye Vyuo husika, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ‘UDSM’ wamebainisha mfumo wanaoutumia kudahili wanafunzi.
Mkurugenzi wa Shahada za Awali, Allen Mushi amesema Chuo hicho kimejipanga vizuri kutekeleza agizo la Serikali kuvitaka Vyuo Vikuu nchini kuwadahili Wanafunzi moja kwa moja Vyuoni badala ya awali ambapo zoezi hilo lilisimamiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, TCU.
“Tumejipanga na tunaendelea na suala hili kwamba Wanafunzi wanaomba moja kwa moja kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanaomba kupitia mtandao wa Chuo ambao upo kwenye website.
“Maelezo yote ya kutumia mtandao huu yanapatikana kwenye tovuti ya Chuo, kuna kitabu kidogo cha Chuo kinachoelezea program zote tulizonazo, vigezo vya kuingia Mwanafunzi.” – Allen Mushi.
PLAY kwenye hii VIDEO hapa chini kutazama kila kitu…
ULIPITWA? Alichokizungumza JPM wakati wa uzinduzi wa hostel UDSM…tazama kwenye video hii kwa kubonyeza play.
ULIIKOSA? UDSM yaongea kuhusu ishu ya vyeti vya Waziri wa sheria…tazama kwenye hii VIDEO!!!