Leo July 31, 2017 Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kupitia Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe imekutana na Waandishia wa Habari katika mkutano uliofanyika Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, CHADEMA imetoa taarifa ya maazimio baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho kukutana kwa siku mbili mfululizo July 29-30, 2017 katika Hotel ya Double Tree, Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zao.
"Serikali ituambie ina mpango gani wa muda mfupi kuokoa hali yetu ya kiuchumi"-Mbowe pic.twitter.com/6JQ7bAyQYY
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Hatuchukii mapambano ya kutafuta haki kwenye rasilimali zetu lakini ufanyike utafiti wa kutosha"-Mbowe pic.twitter.com/fvrIC6SGWF
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Kwa sababu tumeshindwa kuzalisha ndani, Serikali inakopa sana nje bila kujua nani atalipa"-Mbowe pic.twitter.com/zHRTVV0pq2
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Kitu pekee ambacho kimeongezeka kwa kuingizwa nchini ni chakula"-Mbowe pic.twitter.com/A5ZDf5dm5D
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Takwimu za benki kuu zinasema kuwa kwenye benki za biashara Viwanda vimekopa 0%"-Mbowe pic.twitter.com/S11SueSdMQ
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Viwanda vingi vimefungwa kwa sababu ya kodi mbaya hazilipiki, gharama ya kufanya biashara TZ ni maumivu makubwa sana"-Mbowe pic.twitter.com/IrsmK4q87c
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Viwanda vingi vilishindwa kuendeshwa kwa sababu vingi vilikuwa na teknolojia ya zamani"-Mbowe pic.twitter.com/nNho2r8wIh
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Viwanda ambavyo vilibinafsishwa vilikuwa vinaendeshwa kwa hasara"-Mbowe
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Viwanda vingi vilifungwa kwa sababu vilishindwa kujiendesha"-Mbowe pic.twitter.com/CNxZAdHvgs
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye atapewa kitega uchumi ambacho kinamuongezea faida akaamua kukifunga sababu anaichukia TZ"-Mbowe pic.twitter.com/w0nNKbNJmo
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Si kweli kila mfanyabiashara ni mpiga dili"-Mbowe pic.twitter.com/XinXNtWZUM
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Tutaambiwa uchumi unakua lakini umasikini unaongezeka, uchumi unakua mifukoni mwa wale walioko kwenye sekta ambazo zinakua sio kilimo-Mbowe pic.twitter.com/Heln3wSwfm
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Wakati nchi nyingine zinasaidia wananchi kuzalisha vyakula lakini Serikali yetu inapunguza"-Mbowe pic.twitter.com/T9ztnz3vrh
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii miwili vitu vimepanda bei lakini kipato cha wananchi hakijaongezeka"-Mbowe pic.twitter.com/zNdLgPuB46
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Usalama wa taifa ni usalama wa chakula, kama hakuna usalama wa chakula hakuna usalama wa Taifa"-Mbowe pic.twitter.com/G8jWjNDhjA
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Wafanyabiashara wanapolia uchumi unaporomoka, ni kweli unaporomoka"-Mbowe pic.twitter.com/fSoEyHN0wQ
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Leo tutatumia taarifa za benki kuu, hatuna mashaka kwa kuwa taarifa za benki kuu ndio taarifa za Serikali"-Mbowe pic.twitter.com/FRUwejWp95
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Leo tutazungumzia kuhusiana na hali ya uchumi wa nchi yetu"-Mbowe pic.twitter.com/KXPcsaBOPx
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
ULIPITWA? Tundu Lissu afunguka ishu ya kutaka kupimwa mkojo na mengine…play kwenye video hii!