Ni taarifa nyingi ambazo zimekua zikipokelewa na Watanzania kupitia Magazeti, mitandao na hata redio wakati mwingine ambapo moja ya stori ambazo siwezi kuzisahau kwa 2013 ni ile ya Watanzania hamsini kudaiwa kunyongwa kwenye magereza mbalimbali ya China kutokana na kukamatwa na dawa za kulevya.
Hili ni swali langu la kwanza kwa balozi wa Tanzania huko China ambae amenijibu hivi >>> ‘hakua kitu cha namna hiyo, toka nimeanza kufanya kazi ya ubalozi hapa China sijawahi kuona au kusikia taarifa za kunyongwa kwa Mtanzania’
Balozi ameiambia millardayo.com kwamba Watanzania wanaoshikiliwa kwenye magereza mbalimbali hawazidi mia mbili ila wanazidi mia moja na kusisitiza kwamba Ubalozi una majina yao na tayari wameshawatembelea, uko utaratibu wa Magereza wenyewe kupeleka kwa Ubalozi taarifa za kila Mtanzania wanaemshikilia.
Anasisitiza kwamba Watanzania hawa hupewa nafasi ya kuongea na ndugu zao nyumbani Tanzania, vitendo vya watu kukamatwa kwa makosa mbalimbali na kusema wao ni raia wa Tanzania vimekua vikitokea ambapo Ubalozi umekua ukienda ili kuwatambua lakini wanagundua baadae kuwa sio Watanzania, walisingizia tu.