Siku moja imepita toka mitandao na vyombo vya habari vya Ulaya viripoti mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar kuwa amesafiri jana August 2 kuelekea Paris kwa ajili ya kukamilisha dili la kujiunga na Paris Saint Germain.
Neymar ambaye anatakiwa ailipe au club inayomtaka iilipe FC Barcelona dau la pound milioni 199 ambazo ni zaidi ya Bilioni 580 za Kitanzania ili kuvunja mkataba kwa mujibu wa kipengele kilichopo katika mkataba wake na Barcelona, leo dili hilo limeshindwa kukamilika kutokana na LaLiga kukataa.
LaLiga wameripotiwa kukataa malipo hayo ya kuvunja mkataba wa Neymar ambapo wanasheria wake pamoja na wanasheria wa PSG walienda katika ofisi za LaLiga jijini Madrid Hispania lakini dau lao likakataliwa kupokelewa kwa kudai wanavunja sheria za UEFA(Financial FairPlay)
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)