Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.
Nje ya Mahakama hiyo baada ya kesi Wakili Mashaka Ngole amezungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa Mahakama imetoa uamuzi wa kutupilia mbali pingamizi la Wabunge hao wanaowapinga Wabunge wateule wasiapishwe.
Ngole amesema kutupiliwa kwa pingamizi hilo kunatokana na sababu kwamba Jaji Mwandambo alisema kifungu kilichotumiwa na Wabunge hao kuweka zuio sio sahihi hivyo kutokana na hatua hiyo, Wabunge 8 wateule wanaweza kuapishwa muda wowote.
Wakili Ngole amesema kutupwa kwa pingamizi la wabunge waliofutwa CUF ni kwa sababu kifungu kilichotumiwa kuweka zuio sio sahihi. pic.twitter.com/GwJVw404cX
— millardayo (@millardayo) August 4, 2017
ULIPITWA? Wanachama wa CUF walivyopigana ndani ya Mahakama Kuu leo…tazama kwa kuplay video hii!!!