Moja ya vitu ambavyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amevizungumza siku ya August 3, 2017 alipokutana na wasanii wa muziki wa bongo fleva kwa lengo la kusikiliza kero zao ili kujua namna kutafuta sheria mpya za kulinda haki zao.
Waziri Mwakyembe amewaasa pia wasanii kuwa endapo wanataka kufanikisha malengo yao wanatakiwa kuwa na umoja na kuweka kando tofauti zao za zamani huku akiwataka BASATA kujirekebisha katika utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mpya zitakazowasaidia wasanii kukuza na kulinda muziki wao.
>>>”Hatua ambazo Wizara inazichukua na kupata maoini mengine kutoka kwenu. Tufanye nini kwenda mbele, kwa sababu hatuwezi kuendelea kuimba nyimbo zile zile za matatizo wakati tunao uwezo wa kuyatatua mengi tu. Mjadala huu tuongee tu ukweli ‘Tufanye nini kama Serikali?’. Tumekusanya hizi mada zote na wataalamu wangu watanionyesha kila kitu na tutakaa weekend yote hii tuangalie tutafanya nini halafu tutawaita tena.” – Waziri Mwakyembe.
KING MAJUTO KAFUNGUKA: “Nimezushiwa kifo mara 5, lazima nife lakini…”