Mwenyekiti wa zamani wa chama cha soka mkoa wa Pwani na club ya Dar es Salaam Young Africans mwanasheria Iman Madega ni miongoni mwa wagombea Urais wa TFF waliyozindua kampeni zao za kuomba kura za Urais leo kupitia vyombo vya habari.
Iman Madega ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea na anakampuni yake, ameomba kura na kunadi sera zake akidai kuwa wakimpa nafasi ya kuwa Rais wa TFF atachukua likizo ya kazi yake ya uanasheria ili kulitumikia soka pekee maana mpira wa miguu kwa sasa unahitaji muda zaidi.
“TFF ni taasisi nyeti na mpira sasa hivi sio tena wa ridhaa ni kazi ambayo ya masaa 24 hicho kitu nilikiona wakati nipo Yanga, sasa hivi watu wanataka kuuchezea kutoutendea haki mpira wa miguu ili uongoze TFF lazima uwe na muda wa kutosha kuutumikia”– Madega
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0