Siku mbili kuelekea Mkutano Mkuu wa Simba SC ambao umepangwa kufanyika August 13, 2017, baadhi ya wanachama wa Klabu hiyo chini ya Bodi ya Wadhamini leo August 10, 2017 wamefungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuzuia mkutano huo.
Wakili wa Bodi hiyo Juma Nassor amesema Bodi ya Udhamini ya Simba SC imewasilisha Mahakamani kesi kupinga wanaokaimu nafasi za uongozi katika Klabu hiyo kuitisha Mkutano Mkuu na kuendelea na maandalizi ya kuibadilisha Klabu kutoka mfumo iliokuwa nao.
>>>”Limepingwa kwa sababu ni utaratibu ambao haukubaliani na Katiba ya Simba ambayo imesajiliwa RITA ambayo imeunda Bodi ya Udhamini ya Klabu ya Simba ambayo ilisajiliwa 1975.” – Juma Nassor.
Tazama kila kitu kwenye hii video hapa chini!!!
ULIPITWA? Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0!!!