Michuano ya Ndondo Cup 2017 imemalizika leo Jumapili ys August 13 2017 kwa kuchezwa mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya Misosi FC watoto wa Tandale wanaosapotiwa na team Clouds360 dhidi ya Goms United watoto wa Gongo la Mboto wakisapotiwa na team Shilawadu.
Mchezo huo wa fainali uliyochezwa katika uwanja wa Kinesi Dar es Salaam umeshuhudiwa na mashabiki mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye, RC Paul Makonda, DC Ally Hapi na mgeni rasmi alikuwa naibu spika Tulia Akson.
Goms United unaweza kusema licha ya kuongoza hadi dakika ya 70 kwa goli 1-0, mzaha wa golikipa wao ulipelekea Misosi FC kusawazisha goli na kufanya mchezo kuamulia kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1, Misosi FC wamekuwa Mabingwa wa Ndondo Cup 2017 kwa ushindi wa penati 5-4.
Alichokiagiza waziri Mwakyembe baada ya kutangazwa matokeo ya Urais na makamu TFF