Makampuni ya biashara yanazidi kuchukua headlines katika soka la Tanzania baada ya kuzidi kujitokeza kuingia udhamini na vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu, tumeona Singida United wamefanikiwa kupata wadhamini zaidi ya watano.
Good news ilyotangazwa leo kwa club ya Ndanda FC ambayo iliyowahi kuyumba mara kadhaa kiuchumi kutokana na kukosa wadhamini, leo August 15 2017 Ndanda FC wamefanikiwa kuingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na kampuni ya Motisun Group kupitia chapa Kiboko.
Udhamini wa Ndanda FC kutoka kwa Motisun Group unalenga kuisaidia club hiyo katika msimu wa 2017/2018, hivyo Ndanda FC wametangaza kuanzia msimu wa 2017/2018 wa Ligi Kuu katika uwanja wa Nangwanda Mtwara yataanza kuonekana mabango ya Motisun Group kupitia chapa ya Kiboko.
Alichokiagiza waziri Mwakyembe baada ya kutangazwa matokeo ya Urais na makamu TFF