Habari za Mastaa

Wema Sepetu Mahakamani tena leo, Wakili wake Tundu Lissu aweka pingamizi (+Pichaz)

on

Wakili wa mrembo Wema Sepetu, Tundu Lissu leo August 15, 2017 amepinga kupokelewa kwa kielelezo cha ushahidi wa msokoto mmoja na vipisi 2 vya bangi Mahakamani, vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema Sepetu.

Lissu amepinga kielelezo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kumuongoza shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima.

Aidha, Lissu amedai kuwa kielelezo cha ushahidi kisipokelewe kwa sababu ndani ya bahasha yenye ushahidi kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi akisema vipisi 2 vyen

Soma na hizi