Leo August 18 2017 Mamalaka ya uthibiti usafiri wa nchi kavu na majini ‘SUMATRA’ imetoa ufafanuzi juu ya taarifa zinazosambaa kupiti mitandao kijamii na baadhi ya vyombo ya habari kuwa SUMATRA kwa kushirikiana na TANROADS pamoja na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wameanzisha operesheni ya kukamata magari yaliyokiuka ukomo wa mwendokasi na kuyatozo tozo za pamoja ambazo jumla yake ni Tsh 200,000.
SUMATRA imesema ukweli wa suala hilo ni kwamba SUMATRA haitozi tozo za pamoja na taasisi yoyote kuhusiana na kosa hilo, wala SUMATRA haihusiki na kutoa adhabu kwa magari ambayo hayafanyi biashara ya kusafirisha abiria au mizigo.
Hivyo SUMATRA imewaomba watanzania kuzipuuzia taarifa hizo na kuwasihii waache mara moja kusambaza ujumbe huo.
VIDEO: Ulikosa hii ya Manusura wa ajali ya basi la Shule ya Lucky Vincent walivyowasili Bonyeza play hapa chini kutazama