Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) limekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya waumini wa dini hiyo ya kuvamia na kupora misikitini na kusbabisha uvunjifu wa amani,akitoa salam za baraza hilo kwenye Baraza la Maulid lililofanyika mjini Kigoma, Naibu Katibu
Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Mohamed Khamisi amesema kuwa vitendo vya uporoaji wa madaraka kwenye misikiti na umwagaji damu ni kinyume na muenendo na mafundisho ya dini.
Kutokana na hilo amesema kuwa baraza hilo halina budi kukemea kwa nguvu vitendo hivyo na kuwaonya waislam kuacha mara moja kwani vimekuwa vikiipaka matone na kuunajisi uislam.
Akizungumzia jambo hilo kwa niaba ya serikali Mkuu wa mkoa Kigoma, Issa Machibya amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika kuhusika katika vitendo vya uporaji madaraka na kufanya mapinduzi kwenye
misikiti na kupelekea uvunjifu wa amani na umwagaji damu.