Baada ya Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo Alhamisi ya August 24 2017 mjini Monaco Ufaransa kuchezesha droo ya hatua ya makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, walitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017.
Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017 kwa kumshinda mpinzani wake mkubwa Lionel Messi wa FC Barcelona na golikipa wa Juventus Buffon.
Ronaldo kwa msimu wa 2016/2017 ambapo ameshinda pia tuzo ya mshambuliaji bora 2016/2017, alikuwa na msaada mkubwa kwa club yake ya Real Madrid msimu uliyomalizika lakini ameifungia magoli 12 na kutoa assist 6 katika michuano ya UEFA Champions League.
Kiungo Luca Modric wa RealMadrid ndio ametajwa kuwa kiungo bora wa msimu wa 2016/2017 wa #UCL #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/xnbhZZgZRF
— AyoTV (@AyoTV) August 24, 2017
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos ametangazwa kuwa beki bora wa msimu wa 2016/2017 #UCL #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/1I6xnqjgD9
— AyoTV (@AyoTV) August 24, 2017
Kipa wa Juventus Gianluigi Buffon ndio golikipa bora wa msimu wa 2016/2017 #UCL #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/JxgQblLRxb
— AyoTV (@AyoTV) August 24, 2017
VIDEO: Penati ilizoipa Simba Ubingwa wa Ngao ya Hisani vs Yanga