Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwakili ya IMMMA, Sadoc Magai ameelezea kilichotokea katika ofisi yao baada ya kudaiwa kulipuliwa akisema alipata taarifa za tukio hilo saa 11 alfajiri na baada ya kufika ofisini hapo alikuta tayari Jeshi la Polisi likiendelea na shughuli zake.
Amesema kuwa chanzo cha tukio hilo hakijajulikana lakini alikuta mapipa ya Petrol, pia vioo vimepasuka na mlango mkubwa wa kuingilia ofisini humo umebolewa kwa kitu kinachoonekana ni mlipuko.
Hata hivyo, eneo hilo lina walinzi wawili ambao wamekutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui mithili ya watu walioleweshwa.
>>>”Hakuna majeruhi na hakuna kilichoibiwa zaidi ya athari za jengo, ambapo jengo hili lina ofisi za mawakili 25.” – Sadoc Magai.
Polisi walivyomzuia Wakili Fatma Karume kuzungumza baada ya Lissu kuachiwa…tazama hapa chini!!!