Leo August 27, 2017 Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika ‘TLS’, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amelaani kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa Ofisi za Wanasheria IMMMA Advocates huku akisema kuwa Baraza la chama hicho limewataka Mawakili wote ambao ni wanachama kususia kwenda Mahakamani August 29 na 30, 2017.
Aidha, Lissu amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutumia mamlaka ya kiupelelezi kuhakikisha shambulio la mabomu dhidi ya ofisi hizo linachunguzwa kwa kina huku akidai kuwa kitendo hicho kinakiuka sheria na mikataba ya Kimataifa ambayo nchi imeridhia.
>>>”Mawakili wa IMMMA zinawakilisha wateja wa aina mbalimbali zikiwemo kampuni binafsi ya ndani na nje ya nchi, wanasiasa na watu binafsi”. – Tundu Lissu.
TUNDU LISSU KAFUNGUKA CHANZO KUTEKETEA OFISI YA FATMA KARUME
OFISI YA FATMA KARUME YATEKETEA: NINI CHANZO?