Leo August 31 2017 kesi ya Mwigizaji Wema Sepetu kuhusu bangi iliendelea tena kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo mpaka mwisho Mahakama hiyo ilikataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro >>> “Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani“
Hiyo imekua habari njema kwa Wema Sepetu na wengine walie upande wake ambapo baada ya maamuzi hayo ya Mahakama Wema Sepetu alionekana mwenye furaha na kukumbatiana na wafuasi wake akiwemo Mama yake mzazi.
Alichokisema baada ya kutoka Mahakamani ni hiki >>> “nimefurahi kwasababu naona kabisa kwamba haki inatendeka, nawashukuru Mawakili wangu, tunasubiria hiyo siku September 12″
PLAY HII VIDEO HAPA CHINI UJIONEE KILA KITU KILICHOENDELEA LEO
VIDEO: Wema Sepetu asema Alikiba na Diamond ni wendawazimu, play hii video hapa chini kumtazama mwanzo mwisho
VIDEO: Hatimae Jackline Wolper afunguka kuhusu kuachana na Harmonize, Sarah katajwa humo ndani mwanzo mwisho
HAUTAKI KUPITWA??? Kuna hii APP MPYA YA MILLARD AYO kwa wewe wa ANDROID unaweza kubonyeza hapa moja kwa moja kwenda kui-download mtu wangu, HABARI ZOTE KIGANJANI MWAKO >>> APP MPYA BONYEZA HAPA