Naibu Waziri wa zamani wa Kazi na Ajira, Dr. Makongoro Mahanga amefunguka kuhusu ishu yake iliyokuwa imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo ilikuwa inadai kuwa alikamatwa na Jeshi la Polisi.
Dr Mahanga ambaye alikuwa Mbunge wa Segerea na kuteuliwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kustaafu shughuli za kiserikali, sasa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala amedai kusikitishwa na taarifa iliyokuwa inasambaa kwenye mitandao ikidai alikamatwa na Polisi.
>>>”Ilikuwa siku ya kesi, isipokuwa nilipigiwa na RPC kwamba ameitwa kwa hiyo nilipotoka nyumbani ikabidi nipitie kwake kwamba mbona leo ndiyo tarehe 31 ambayo ndiyo siku ya kesi? Nikamwambia mbona mimi ninayo akasema basi twende. Kwa hiyo tulikuja nayo kwenye gari yangu.” – Dr. Makongoro Mahanga.
Maneno ya Wema Sepetu nje ya Mahakama baada ya vielelezo kukataliwa
TAMKO LA CHADEMA: Ni kuhusu taarifa za Mbowe kufuta mchakato