Baada ya Mahakama Kuu Kenya leo September 1 2017 kutangaza kubatilisha matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya uliyompa ushindi Uhuru Kenyata dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, wengi walikuwa na hamu ya kufahamu Uhuru Kenyata atasema nini.
Uhuru Kenya ambaye alitangazwa mshindi wa Urais katika uchaguzi Mkuu wa Kenya August 8 2017, binafsi hakubaliani na maamuzi hayo ya Mahakama lakini kwa mujibu wa sheria ana heshimu na kukubali kwani hataki kuona Kenya ikiingia katika machafuko.
“Ushindi wangu ulikuwa ni matakwa ya watu lakini tunaamini katika utawala wa kisheria, siku zote jirani zako watabaki kuwa ni jirani zako tu hata iweje” >>> Uhuru Kenyata
Kwa maana hiyo basi uchaguzi Mkuu wa Kenya kwa mujibu wa katiba ya nchi yao, utafanyika upya ndani ya siku 60 kama alivyotangaza jaji Mkuu David Maraga mapema leo baada ya taarifa za ubatilishaji wa matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
ULIPITWA: CCM yaongelea maamuzi ya Mahakama Longido…tazama kwenye hii video!!