Moja ya headline iliyochukua nafasi August 31, 2017 ilikuwa ni pamoja na hii taarifa kutoka Tanga ambayo ilidai kuwa Madiwani watano wa CUF wamesimamishwa kutohudhuria vikao vitatu na kukatwa posho ya vikao vinne kwa kosa la kwenda kujisaidia wakati Mbunge akizungumza.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruku kupitia CUF na kueleza hali ilivyokuwa hata ikachukuliwa hatua hiyo akisema kuwa si kwamba wameadhibiwa kwa kwenda kukojoa bali ni kutokana na utovu wa nidhamu wanaouonesha kwa Mbunge huyo mara kwa mara.
>>>”Sio kwenda kukojoa, kufanya hivi si mara ya kwanza. Hili ni tukio karibu la mara ya tatu wamelirudia na Mstahiki Meya amekuwa anawaonya kwamba hawamuwezi kutoka Madiwani nane wote mkasema mnaenda kujisaidia, haiwezekani.
“Hili jambo linajulikana kwamba ndani ya CUF katika Wilaya ya Tanga kuna sintofahamu kwamba Mwenyekiti mpaka leo anasema hamkubali Mbunge na wengine amewashika masikio. Sijui ni Madiwani wa namna gani kwa sababu wamechaguliwa katika Kata zao, wawakilishi wa wananchi waliowachagua na katika Halmashauri ya Wilaya akiwaambia tokeni nje wanatoka, fumbeni macho, wanafumba.” – Mbunge Mussa Mbaruku.
ULIPITWA? Maamuzi ya Mahakama Kuu ile kesi ya Wabunge 8 waliofutwa CUF…tazama hapa kenye hii video!!!
ULIPITWA? MAHAKAMA KUU KUHUSU WALE WABUNGE 8 WA CUF!!!