Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Jumatatu ya September 4 2017 iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kamati ya watu watano watakaosimamia uuzwaji wa hisa za club hiyo kwa muwekezaji, baada ya kuafiki kuingia katika mfumo wa hisa.
Simba baada ya kutangaza majina hayo, mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano wa club hiyo Haji Manara alitangaza kuomba msaada kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kupiga vitaa uuzwaji wa jezi feki kama alivyofanya kwa watu wanaouza CD feki za wasanii.
“Kwa muda wa miaka miwili club ya Simba pasipokuwa na mashaka ukiona jezi tu ile unasema hii ni jezi ya Simba sizungumzii rangi nazungumzia hii jezi unaijua hii ni jezi ya Simba lakini bado tuna tatizo la watu kufyatua jezi feki, Simba tunauza jezi kupitia matawi na mawakala”>>> Haji Manara
“Niombe mamlaka zinazohusika maana sisi hatuna jeshi na hatuna mamlaka kufunga watu na hasa katika hili nimuombe mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda kuna wakati fulani alisaidia sana sana kupiga vita uuzwaji wa kazi feki za wasanii”>>> Haji Manara
VIDEO: Simba wamefikia huku kuhusu ile ishu ya uuzwaji wa hisa