Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo September 4, 2017 katika mchakato wa kuboresha huduma za afya nchini, amezindua huduma za matibabu bure kwa wazee katika Manispaa Ubungo ambapo Wazee 7,299 wamepatiwa vitambulisho vya huduma za afya bure ndani ya Manispaa hiyo.
Waziri Mwalimu ameelekeza kuwa Wizara yake inaendelea na mazungumzo na Wizara ya Fedha kuona namna ya kuwasaidia wazee na watu wasio na uwezo kifedha katika kupata kipaumbele kwenye huduma za afya katika kuwapatia bima afya.
>>>”Vitambulisho hivi vya matibabu ni hatua ya awali na lengo kuu ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata bima ya afya ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini.” – Waziri Ummy Mwalimu.
WAZIRI UMMY! “Hatukatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya Dawa lakini…”
Ulipitwa? SHAMBULIZI LA CHUI: Majeruhi asimulia alivyonusurika kuuawa