Kampuni ya kutengeneza magari Nissan hivi karibuni imetengeneza na kuzindua aina mpya ya magari ambayo yanatumia umeme yanayo fahamika kama ‘Leaf’.
Magari hayo yanaweza kusafiri mwendo wa hadi asilimia 50 zaidi ya yale yaliyopo sasa baada ya kupata chaji na yana mfumo wa kujiendesha unaofahamika kama ProPilot Park, ambao huyawezesha kupenya maeneo magumu hususani wakati wa kuegeshwa.
Magari haya pia yanaelezwa kuwa na teknolojia ya kujiendesha yenyewe hasa kwenye barabara ambayo inaelekea upande mmoja tu na yataanza kuuzwa Japan mwezi Oktoba kabla hayajaanza kuuzwa sehemu nyingine duniani mwaka 2018.
Ulipitwa na hii? Tanzania imekuja na hii teknolojia ya App inayokupa habari hata ukizima data
Hii je? KWA MARA NYINGINE: Treni ya kifahari ya Rovus yaja DSM