Viongozi wa Chadema leo September 8, 2017 wameongea na waandishi wa habari kuhusu shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu lillilotokea jana mchana mjini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine waliyoyazungumza, haya ni mambo 10 makubwa
"Tunawashukuru wote waliokuwa eneo la tukio kwa sababu cha kwanza kilichokuja kwenye akili yao ni kuokoa maisha ya Lissu." #ChademaPRESS
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Alipelekwa Hospitali ya Dodoma, tunawashukuru sana Madaktari kwa jitihada zao za kuokoa maisha yake mpaka leo Lissu ni hai." #ChademaPRESS.
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Najisikia niko protected kwa sababu nina hiyo professional. Mungu awabariki sana Madaktari waendelee na moyo huo" #ChademaPRESS.
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Damu ya Lissu imemwagika nyingi sana, baada ya kupewa taarifa za shambulio nilikosa cha kusema nilipoambiwa idadi ya risasi." #ChademaPRESS
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Mwenye maamuzi ya kuchukua uhai wa mtu ni Mwenyezi Mungu sio binadamu. Hawatafanikiwa na hawajatutisha, wametuimarisha." #ChademaPRESS.
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Kwa kuwa damu ya Lissu imekanyaga ardhi kabla ya wakati wake, niwaombe Makamanda twende ktk Hospitali zetu tukachangie damu" #ChademaPRESS
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Na damu hii iwe ishara tosha kwamba sasa tuko tayari kulikomboa Taifa." #ChademaPRESS.
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Kwa hiyo nategemea kuanzia leo nitakuwa nikipokea taarifa za jinsi Makamanda mnavyojitolea kwenda hospitalini kuchangia damu" #ChademaPRESS
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Ili kuhakikisha tunakuwa na umoja na Tundu Lissu anapata huduma bora za matibabu wanachama wengi wamejitoa uchangia chochote" #ChademaPRESS
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
"Nawaomba Makamanda wote tulitoa ratiba za vikao lakini kwa udharura huu mkutane kujadili hali ya usalama ktk maeneo yenu." #ChademaPRESS
— AyoTV (@ayotv_) September 8, 2017
BUNGENI! TAARIFA YA SPIKA KUHUSU LISSU “Risasi kati ya 28-32 zilitumika”