Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa leseni kwa vituo 32 vya Televisheni hapa nchini ikiwa ni kuongeza muonenoano na usikivu katika maeneo mbalimbali.
Akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Vijijini, Martin Alexander Mtonda ambaye alitaka kujua idadi ya vituo virushavyo matangazo kwa njia ya Television na Makampuni yanayomiliki vituo hivyo, Naibu Waziri wa Habari Anastazia Wambura amesema vipo vituo 32 ambavyo vimepewa leseni ya kurusha matangazo kwa njia ya Television.
Baadhi ya vituo vilivyosajiliwa ni ITV, Star TV, Channel Ten, TBC1, TBC2, East Africa TV, AGAPE Television, C2C, Dar es Salaam TV ‘DTV’, Aboud Television, CTN Television, Capital Television, Clouds TV, Sokoine University of Agriculture ‘SUATV’, VIASAT 1 Television, Sibuka TV na Tumaini TV.
Tazama kwenye video hii kuna kila kitu…
RPC Mwanza kaeleza kuhusu ajali iliyojeruhi Askari na Mahabusu