Leo Jumapili ya September 10 2017 muamuzi wa kike wa mchezo wa mpira wa miguu Bibiana Steinhaus ameandika rekodi mpya barani Ulaya kwa kuwa muamuzi wa kwanza wa kike kuwahi kuchezesha mechi ya Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga.
Bibiana Steinhaus mwenye umri wa miaka 38 ameweka rekodi ya kuwa muamuzi wa kwanza wa kike katika Ligi tano kubwa barani Ulaya (Ufaransa, Hispanai, England, Ujerumani na Italia) kuwahi kuchezesha mechi za Ligi Kuu za wanaume.
Mchezo wa Hertha Berlin dhidi ya Werder Bremen wa Bundesliga uliyochezwa leo na kumalizika kwa sare ya 1-1, ulichezeshwa na Bibiana Steinhaus ambaye nje ya urefa ni askari Polisi, mchezo wa leo ndio mkubwa wa wanaume aliyowahi kuuchezesha.
Bibiana ameanza kazi ya uamuzi toka mwaka 2007 hadi kufikia hapo amechezesha michezo zaidi ya 80 ya Ligi daraja la pili, amechezesha fainali ya wanawake ya Champions League 2017 na michuano ya wanawake ya Olympic 2012 London lakini tegemea kuendelea kumuona Bundesliga wa 2017/2018 akichezesha mechi kadhaa.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0