Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu headlines za tetemeko la ardhi Kagera ambalo lilitokea September 10, 2017 na kusababisha athari kubwa kwa wananchi ikiwa pamoja na vifo vya watu 17, uharibifu wa miundombinu ambapo katika kumbukumbu hiyo baadhi ya wananchi wameeleza jinsi maisha yalivyo tangu lilipotokea tetemeko hilo.
Wakiongea na Ayo TV na millardayo.com Wananchi hao wamesema baadhi yao wanalala nje hadi sasa huku wengine wakilazimika kuuza viwanja na kukopa fedha ili kuweza kurudisha nyumba zao na kuongeza kuwa pamoja na misaada iliyopokelewa Serikalini haikuwasaidia kama walivyotegemea.
Wananchi hao wameelekeza kilio chao kwa Serikali kuwasaidia kurudisha miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko na kuwasiadia wanaolala kwenye mahema kupata makazi ya kudumu kwa kuwa wanakutana na changamoto kubwa pindi mvua zinaponyesha na usalama wa mali zao kuwa hatarini.
ULIPITWA? Familia zilivyolala nje Bukoba Sept. 11 kuhofia tetemeko la ardhi kurudi