Tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu na watu wasiojulikana linaendelea ku-make headlines huku Vyama vya siasa, taasisi, viongozi wa dini, viongozi wa Serikali na wanaharakati wa Haki za Binadamu wakionesha kukemea tukio hilo na miongoni mwao ni Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) ambacho kimetoa tamko pia.
Katika mkutano na Wanahabari uliofanyika katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Buguruni DSM ADC kupitia kwa Katibu Mkuu wake Doyo Hassan Doyo kimetoa tamko la kulaani tukio lililomtokea Mbunge huyo na Mwanasheria wa CHADEMA na kutoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu Usalama wa wa raia pindi anapotoa taarifa za kufuatiliwa na watu wasiojulikana.
>>>”Chama chetu cha ADC kinalaani tukio la kinyama la kupigwa risasi ndugu yetu Tundu Lissu lililotokea Dodoma. ADC tunalaani vikali tukio hilo.” – Doyo Hassan Doyo
EXCLUSIVE: Mdogo wake Tundu Lissu azungumzia tukio la Lissu kushambuliwa