Rais John Magufuli leo September 11, 2017 amemwapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam ambapo Rais Magufuli alipata nafasi ya kuhutubia na miongoni mwa aliyozungumza ni pamoja na haya mambo kumi makubwa.
"Naungana na wananchi wote kukupongeza Jaji Prof Ibrahim Juma kwa kuchaguliwa kwako kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, hongera sana." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Moja lililo kubwa, sikutaka kumteua Jaji baada ya mwaka mmoja nateua tena Jaji au baada ya miaka miwili anastaafu niteue tena" @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Nilitaka nikiteua Jaji akae hata miaka 10. Niliyazingatia hayo na mengine mengi ikiwemo historia na dhamira yangu inaridhika." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Lengo ni kumpata Jaji Mkuu ambaye atakaa muda mrefu mpaka atakapoamua Mungu katika kipindi cha kuanzia miaka 7, 8 au 10." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Bajeti ndogo, marupurupu, usafiri. Changamoto ni nyingi na nakuhakikishia Jaji Mkuu, mimi pamoja na Serikali tunafahamu." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Tunafahamu changamoto kwenye maeneo mengine, Bungeni, Polisi, Jeshini, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto, PCCB pia." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Ukishakuwa kiongozi katika nchi masikini kama Tanzania ni lazima uzikubali changamoto." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Nimekupongeza na nawapongeza Majaji na Mahakama, mnafanya kazi nzuri." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Tembeeni vifua mbele mkijua Serikali tunatambua kazi nzuri. Kazi nzuri siku zote kutakuwa na watu wa kuwasota." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
"Wanasema mwembe wenye matunda ndio unapigwa mawe sisi tutapondwa na nyinyi mtapondwa. Ndio taratibu za watu waliozoea kuponda" @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 11, 2017
“Wastaafu wengine hawachoki kusema, wanawashwa” – Rais Magufuli
ULIPITWA? “Sikuja kutafuta Mchumba” – Rais Magufuli
Hii je? Rais Magufuli atinga kanisani kwa Wasabato Magomeni, awapa pesa