Bado Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 mbichi na kwa namna ilivyo huwezi kutabiri ni timu ipi inaweza kuwa bingwa wa Ligi Kuu lakini cha kushangaza leo September 11 club ya Crystal Palace imetangaza kuachana na kocha wake mkuu Frank de Boer.
Crystal Palace imefikia hatua ya kumfuta kazi Frank de Boer leo na nafasi yake inaripotiwa kuwa itatangazwa kurithiwa na Roy Hogson ndani ya saa 24, kufutwa kazi kwa Frank de Boer kumewashitua wengi baada ya maamuzi hayo kuja siku 77 baada ya kocha huyo kujiunga nao.
Frank de Boer anakuwa kocha wa kwanza msimu wa 2017/18 England kupoteza ajira yake akiwa kaiongoza Crystal Palace katika michezo minne na kupoteza yote akiwa kapewa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya pound milioni 2 kwa mwaka lakini anakuwa kocha aliyedumu na club kwa muda mfupi.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0