Ni kawaida kuona shughuli za upigaji picha wa passport size za dakika tatu zinafanyika katika ofisi maalumu, kwenye mazingira yenye umeme au jirani na eneo lenye umeme.
Katika hali ya kushangaza na kufurahisha nimekutana na kijana wa miaka 19 Kahama anayepiga picha hizo za passport size chini ya mwembe huku akiwa ameshikiza kitambaa kinachowekwa nyuma ya mpigwa picha kama background kwenye kiti cha kupigia picha hizo ambacho ndicho anachokalia anayepigwa picha.
Kijana huyo anayeitwa Elia ambaye alihama kutoka Kigoma kuja Kahama kutokana na kukatisha masomo yake baada ya kutofanya vizuri na wazazi wake kushindwa kumuendeleza aliamua kuanza biashara ya kuuza karanga ambayo ndiyo iliyompatia mtaji wa kuanzisha biashara hiyo ya kupiga picha.
Bonyeza PLAY hapa chini kupata taarifa kamili..
Mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali