Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai leo September 14 2017 akiwa Bungeni Dodoma kazungumza na kujibu tuhuma za Mbunge wa Arusha Godbless Lema kuhusu kudai Bunge kutogharamia matibabu ya Mbunge Tundu Lissu aliyepo Nairobi.
Spika Ndugai ameeleza na kufafanua kuhusiana na taratibu za Mbunge ili alipiwe matibabu na mwisho akatangaza yeye kama Spika ameamua kumsamehe tu Godbless Lema kwa kauli zake, baada ya taarifa hizo kumfikia Lema ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa
“Mh Spika nashukuru kwa msamaha wako wa bure lakini Mimi na familia yangu tumechagua kuendelea kukuombea“>>> Lema
VIDEO: SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AKIJIBU TUHUMA ZA GODBLESS LEMA DHIDI YAKE KUHUSU TUNDU LISSU