Rais John Magufuli yupo kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Manyara ambapo leo September 20, 2017 alipata nafasi ya kuwahutubia Wananchi wa Simanjiro. Kati ya mengi aliyoyazungumza akiwa anazungumza na wakazi hao wa Simanjiro, JPM amezungumza mambo haya 15 makubwa
"Kuna changamoto nyingi zinazolikabili Taifa hili, nyingine tumezileta wenyewe tumeshindwa kusimamia rasilimali zetu" @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Nchi hii ni tajiri nanyi ni mashahidi. Historia ya Dunia inazungumza wazi, Watanzania tulipendelewa na Mwenyezi Mungu" @MagufuliJP #Manyara
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tukapewa madini ambayo hayapo popote duniani. Sio Marekani, Uingereza wala Urusi hakuna madini yanayoitwa Tanzanite." @MagufuliJP #Manyara
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Yanachimbwa Mererani, lakini tujiulize Watanzania madini yanatunufaisha? Mungu ametupa madini lakini tunapata shida" @MagufuliJP #Manyara
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tumemkosea nini Mungu? Tulimkosea nini Mungu? Hilo ndilo somo langu la leo." @MagufuliJP #Manyara
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tanzania matatizo yetu sio vyama, matatizo yetu ni kwa nini tunaibiwa." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tanzanite hii kama ingepewa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Inawezekana Mungu alifanya makosa akaweka Tanzanite kwa Watanzania." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tanzanite yote inayochimbwa hapa Serikali na Wananchi wanapata faida 5% nyingine zinawanufaisha wengine nchi nyingine" @MagufuliJP #Manyara
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tanzanite ingekuwa inatumika vizuri na madini mengine kusingekuwa na matatizo ya barabara." @MagufuliJP #Manyara
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Nawaomba Watanzania tusimame imara. Tulipoanza vita dhidi ya mafisadi lazima twende pamoja." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Ndugu zangu maendeleo hayana chama, mtaanza kugombana wenyewe kwa sababu ya vyama, mnachelewa. Adui yetu sio huyo." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Mtang'ang'ania ya pembeni mkaacha ya muhimu. Viongozi wangesimamia vizuri Tanzanite Tanzania isingekuwa masikini." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Kubwa linalofanyika, viongozi tunaopewa mamlaka ya kusimamia haya tunakuwa sehemu ya mafisadi wa kuwaumiza Watanzania masikini" @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
"Tunasahau tulikotoka, tunasahau tulipo na tunasahau tunapokwenda." @MagufuliJP #Manyara.
— AyoTV (@ayotv_) September 20, 2017
Ulipitwa na hii? “Wastaafu wengine wana washwawashwa” – RAIS MAGUFULI
Hii je? “Sikuja kutafuta Mchumba” – Rais Magufuli