PRESIDENT Magufuli leo amewatunuku Kamisheni Maafisa wanafunzi ambapo pia alipata nafasi ya kuwahutubia wananchi walioshuhudia sherehe hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Rais Magufuli kazungumza mambo mengi ya Uchumi na masuala ya Ulinzi na Usalama lakini pamoja kuzungumza mambo mengi nimekusogezea haya 15 makubwa.
"Tumefanya uhakiki kwa wanaosambaza pembejeo, tumekuta kuna pembejeo hewa zenye thamani ya Bilioni 58." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Palikuwa na wanafunzi hewa wa Sekondari na Shule za Msingi 65,000, Kaya hewa za TASAF 56,000, mtu anaitwa masikini kumbe ana maghorofa."
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Kama wapo mafisadi wanaotegemea kula hela za watu waache, watubu, kama wamezificha hizo hela zitawaozea. Tanzania mpya." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Hakuna fisadi aliyenichangi hela kwa hiyo siogopi kumtumbua kwa sababu sikula hela yake, hili la kutumbua watatumbuka kweli" @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Tulianza kushughulikia huu uozo uliokuwa ndani ya nchi. Unaposhughulikia haya masuala usitegemee baadhi ya watu watafurahi" @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Kwa sababu niliingia bila kutoa rushwa na nilikuwa najaribu, sasa lazima nifanye kweli kwa manufaa ya Watanzania wanyonge." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Niliomba Urais wa Tanzania, sijaomba urais wa kutembelea nchi nyingine." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Ukitaka kuwaibia watu unawapumbaza na kuwafanya wagombane wao kwa wao. Mi CHADEMA, Mi CCM, ulipozaliwa hukuwa na chama" – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Baba wa Taifa aliwahi kusema pale ni mateso, mimi nimeyaona mateso ya kuwa Ikulu, niliomba kwa kujaribu nikasukumiziwa huko." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Najua siku moja mtakumbuka, hamuwezi kujua mateso ninayo yapata, ni shida kuwa Rais." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Nimeamua kuwa sadaka kuwanyoosha mafisadi hawa ambao walizoea kuwaibia watanzania." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Itatosha tutapoacha kuibiwa dhahabu yetu, almasi zetu na viongozi wetu watakapokuwa waaminifu na sio mafisadi." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Fedha inawezekana isitoshe, itatosha tutakapojenga uchumi wetu, itatosha tutapoanza kuzuia Tanzanite isitoke." – @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"Mtu ameiba Milioni 100 anampa mtu yeyote analipia hata kiti kwenye Bar, leo hawafanyi hivyo kwa sababu hela imekuwa na thamani" @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
"U hewa hewa upo kila mahali, inawezekana hata kuna mapenzi hewa." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) September 23, 2017
“Hamuwezi kujua mateso ninayoyapata, ni shida kuwa Rais” – President JPM
ULIPITWA? MBOWE KUHUSU WANAOJITOKEZA KUMPELEKA LISSU NJE YA NCHI