Klabu ya Everton ilifanya jaribio la usajili wa rekodi ya klabu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa siku ya mwisho wa usajili wa dirisha la majira ya joto, lakini aliwajibu anataka kurejea Atletico Madrid, kwa mujibu wa gazeti la Marca.
Gazeti hilo la Uhispania limedai kuwa ofa hiyo ilikuwa na thamani ya pound Milioni 66.4 pamoja na bonus ilitumwa kutoka Goodison Park kwenda Stamford Bridge kwa ajili ya mshambuliaji, lakini maafisa wa Everton walijibiwa hajakubali.
Inadaiwa kuwa, ingawa Chelsea walitaka kumuuza mshambuliaji huyo, lakini Costa alikataa kusikiliza ofa yoyote ambayo haikutoka katika klabu yake ya zamani, licha ya usajili wowote usingemruhusu kucheza hadi January.
Dondoo za Diego Costa kwa Chelsea na Atletico Madrid
MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC leo Sept. 21 Mwanza (2-2)