Mwanamke raia wa Misri, Eman Ahmed Abd El Aty, ambaye alifahamika pia kama mwanamke mwenye uzito mkubwa zidi dunia, amefariki akiwa katika Hospitali ya Burjee, Abu Dhabi leo September 25, 2017.
Eman, ambaye alikuwa na uzito wa kilo 500, alidafirishwa kwenda Mumbai, India mwezi February ambako alifanyiwa upasuaji kupunguza uzito chini ya daktari bingwa Dr Mufazzal Lakdawala katika Hospitali ya Saifee, kisha alihamishiwa Abu Dhabi mwezi May baada ya tofauti kadhaa kati ya dada na uongozi wa Hospitali ya Saifee.
Taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Burjee ilisema kwamba Ms Ahmed alivuta pumzi yake ya mwisho alfajiri ya saa 4.35 Jumatatu.>>>”Alikuwa na matatizo kutokana na kulala, ikiwemo ugonjwa wa moyo na tatizo la figo.” Ilisema sehemu ya taarifa ya Hospitali na kuongeza kwamba alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari 20.
Mabula na Mongella wameungana na kuingia mtaani Mwanza