Beki wa club ya Manchester City ya England Benjamin Mendy ameanza safari ya kuelekea jijini Barcelona ambapo anakwenda kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya jeraha lake la goti, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Ulaya vinadai jeraha hilo litamuweka nje kwa muda mrefu.
Mendy ambaye alijiunga na Man City kwa dau la pound milioni 52 akitokea club ya AS Monaco ya Ufaransa, aliumia goti lake la kulia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Man City dhidi ya Crystal Palace, Mendy aliikosa game ya Champions dhidi ya Shakhtar Donetsk iliyomalizika kwa Man City kupata ushindi wa magoli 2-0.
Man City imelazimika kumpeleka Mendy jijini Barcelona kwa ajili ya kuhakikisha jeraha hilo haliwezi kumuweka nje ya uwanja kwa miezi mingi, hata hivyo baadhi ya mitandao leo imeripoti kuwa Mendy atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9.
MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)